Habari zetu? Ninatumaini kwamba mnakuwa na wikendi nzuri sana. Kwa mada yetu ya blogu, ningependa kujua mtafanya nini kwa likizo yetu ya majira ya kuchipua. Ninajua kwamba tunahitjai kupita mitihani yetu bado, lakini nimeshafurahi sana kuwa na likizo fupi kupumzika kidogo.
Kwa likizo yangu, nitaenda kwa muda wa siku moja pale Napa, kunywa vinyo kidogo na kuona mashamba ya mizabibu mbalimbali na rafiki zangu. Halafu, rafiki zangu nami, tutaendesha mpaka California kusini kwenda safari ya burudani. Safari yetu itaenda kisiwa cha Catalina, ambacho kipo karibu na mji wa Los Angeles kiasi fulani, halafu tutaenda Mexico mpaka mji wa Ensenada. Nimefurahi sana kupumzika, kutembelea Mexico (kwa sababu nilitembelea Mexico mara moja tu), na kustarehe na rafiki zangu.
Je, mtafanya nini kwa likizo zenu?
~Furaha
Monday, March 3, 2008
Likizo Fupi (Kutoka kwa Furaha)
Subscribe to:
Posts (Atom)