Wiki hii, nataka kujua aina za sanaa mnapenda kufanya. Pia, ni aina ya sanaa gani mnapenda sana kuona au kusikia? Mimi hupenda kupiga picha za watu na wanyama na dunia. Siwezi kuifanya kila wiki kwa sababu shule ni ngumu, lakini kama unaniona kwa likizo fupi zangu utaona mimi pamoja na kamera yangu. Aina ya sanaa napenda zaidi ni kwenda kuona sinema za kimataifa, na pia napenda kuona picha za wapigapicha wengine.
Zuri
Friday, April 18, 2008
Sunday, April 13, 2008
Meja na Madarasa Mashurutishwa Katika Vyuo Vikuu
Kutokana na mada ya blogu ya Mwalimu kuhusu mahali ya kuishi ya wanafunzi, ningependa kusikia maoni yao kuhusu masomo katika vyuo vikuu, na jinsi ya kuamua meja. Unafikiri wanafunzi wa chuo wanahitaji kuamua meja moja lini? Hapa Stanford, wanafunzi wanahitaji kuamua meja yao kabla ya kumaliza mwaka wa pili. Unafikiri mwaka wa pili ni mapema mno, au sio? Pia, nje ya meja yao, wanafunzi hapa Stanford wanahitaji kusoma madarasa mashurutishwa mbalimbali, kama IHUM, PWR, nk. Unafikiri madarasa mashurutishwa ni muhimu, au sio? Ningependa kusikia maoni yao.
Tutaonana kesho,
Furaha
Tutaonana kesho,
Furaha
Sunday, April 6, 2008
Makazi ya Wanafunzi
Habari za leo?
Nimeamua kuanzisha mada ya kwanza katika blogu yetu muhula huu. Katika mada hii, ningependa kujua maoni yenu kuhusu makazi ya wanafunzi. Nina maswali mawaili. Kwanza, unafikiri ni vyema kwa wanafunzi wa shule za upili kukaa katika bweni shuleni kama wanavyofanya wengi huko Afrika Mashariki au kukaa nyumbani pamoja na wazazi wao kama hali ilivyo hapa Marekani? Pili, unadhani ni bora kwa wanafunzi katika vyuo vikuu kukaa katika mabweni ya chuo au kukaa mjini katika nyumba za kukodisha? Kwa nini?.

Subscribe to:
Posts (Atom)