Monday, March 3, 2008

Likizo Fupi (Kutoka kwa Furaha)

Habari zetu? Ninatumaini kwamba mnakuwa na wikendi nzuri sana. Kwa mada yetu ya blogu, ningependa kujua mtafanya nini kwa likizo yetu ya majira ya kuchipua. Ninajua kwamba tunahitjai kupita mitihani yetu bado, lakini nimeshafurahi sana kuwa na likizo fupi kupumzika kidogo.

Kwa likizo yangu, nitaenda kwa muda wa siku moja pale Napa, kunywa vinyo kidogo na kuona mashamba ya mizabibu mbalimbali na rafiki zangu. Halafu, rafiki zangu nami, tutaendesha mpaka California kusini kwenda safari ya burudani. Safari yetu itaenda kisiwa cha Catalina, ambacho kipo karibu na mji wa Los Angeles kiasi fulani, halafu tutaenda Mexico mpaka mji wa Ensenada. Nimefurahi sana kupumzika, kutembelea Mexico (kwa sababu nilitembelea Mexico mara moja tu), na kustarehe na rafiki zangu.

Je, mtafanya nini kwa likizo zenu?
~Furaha

4 comments:

Zuri said...

Nitakuwa na darasa! Lakini darasa hili itakuwa safi kwa sababu kazi zenu ni kupiga kambi tu kwa Kalifornia kusini. Kuanza nitakuwa na siku mbili kustarehe hapa chuoni. Baada ya siku mbili nitasafiri pamoja na watu kumi na tatu mpaka Big Sur. Tutakaa pale kwa siku tatu na halafu tutaenda mpaka Joshua Tree National Park kwa siku tatu pia.

Nafurahi sana kwa sababu napenda kupiga kambi lakini bado sina nafasi au wakati kuifanya hapa Marekani. Kwa darasa hatupaswi kufanya kitu cho chote, lakini tutaona ardhi na wanafunzi wengi wako wanataka kuwa wageologi (geologists).

Lena said...

Sitakuwa na likizo ya majira ya kuchipua. Nitaendelea kufanya kazi hospitalini na waja wazito na wasichana wenye kansa.

Wikendi iliopita nilienda kuonja vinyo pale ufumbi wa mto wa Kirusi. Tulikunywa vinyo kutoka mapipa badala ya chupa. Pia tulipiga kambi wakati wa usiku wawili. Tumefurahi sana, ingawa kulikuwa na baridi wakati wa usiku. Tulitumia kuni ili tuwake moto.

Upendo said...

Kwa likizo fupi yangu nitafanya shughuli kama Furaha atafanya. Baada ya kumaliza mitihani nitaondoka Palo Alto na rafiki yangu kwenda kufunga safari ya barabara. Tutaenda katika Napa Valley kunywa vinyo na kutembelea mashamba (kama Furaha), kisha tutaenda katika mji wa Las Vegas na Reno pia. Halafu tutaenda katika Park City (jimbo la Utah). Familia yangu tuna nyumba kidogo pale Park City kwa hivyo sisi wawili tutakaa pale kupumzika na labda kucheza thelugini. :) Kisha tutakwenda kutembelea "Arches National Park" na "Grand Canyon." Tutapiga kambi pale. Mwishowe tutafika nyumbani kwangu (hapa Stanford) kulala kidogo na kujiandaa kuanza madarasa mengine. Wakati wote ya likizo hii rafiki yangu nami tunapaswa tutume uombi nyingi sana (ili tupate kazi kwa mwaka ujao). Itakuwa likizo safi sana -- kila kitu ila kufanya kazi wakati wa kujistarehe.

Deshka Foster said...

Sawa jamani, mtaenda kufanya vitu vizuri sana kwa likizo. Hata mimi, kwa likizo fupi mimi na rafiki yangu nzuri, anaitwa Jess, tutaenda Ulaya kutembelea Yakobo (kutoka Stanford na darasa la kuswahili mwaka uliyopita). Anakaa Oxford kusoma kwa Rhodes Scholarship. Itakuwa nzuri sana kwa mimi kuona yeye kwa sababu yeye ni rafiki yangu mzuri mno!

Pia pale UK nitatembelea rafiki yangu anaitwa Neb na yeye amesoma na kaka yangu katika Chuo Kikuu cha Dartmouth. Pia, mtu mwingine tutatemebela ni rafiki yangu anaitwa Galina na sisi wawili tumesoma pamoja katika shule ya secondari.

Nitakaa pale UK kwa siku tisa na nafikiri nita sherehe na rafiki, kuona nchi ya pale na pia kujaribu kufanya kazi katika thesis yangu kwa sababu nitahitaji kumaliza kuindika thesis yangu sasa hivi.