Habari za leo?
Nimeamua kuanzisha mada ya kwanza katika blogu yetu muhula huu. Katika mada hii, ningependa kujua maoni yenu kuhusu makazi ya wanafunzi. Nina maswali mawaili. Kwanza, unafikiri ni vyema kwa wanafunzi wa shule za upili kukaa katika bweni shuleni kama wanavyofanya wengi huko Afrika Mashariki au kukaa nyumbani pamoja na wazazi wao kama hali ilivyo hapa Marekani? Pili, unadhani ni bora kwa wanafunzi katika vyuo vikuu kukaa katika mabweni ya chuo au kukaa mjini katika nyumba za kukodisha? Kwa nini?.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
4 comments:
Kwa shule za upili nafikiri ni vyema kwa wanafunzi kukaa katika bweni shuleni kwa sababu pale wanaweza kuanza kujifunza jinsi kukaa bila wazazi. Kwa shule za upili wanafunzi wa bweni watakuwa na rafiki wengi na watakuwa na wazazi wa bweni.
Pia, nafikiri ni bora kwa wanafunzi katika vyuo vikuu kukaa katika mabweni ya chuo kwa sababu pale wanaweza kusoma pamoja na rafiki wao. Bwenini wanafunzi wanaweza kuwa na chakula kizuri na usalama na wako karibu vyou vikuu vyao.
Nafikiri ni vyema kwa wanafunzi washule za upili kukaa nyumbani pamoja na wazazi wao kwa sababu ni muhimu sana watoto wafundishwe desturi na mila na wazizi wao. Wakiishi katika bweni shuleni, wanajifunza na rafiki, wanafunzi wengine, na walimu badala ya wazazi na ndugu wao. Pia hapa Marekani ni ghali sana watoto wanapelekewa shule ya bweni na shule ya serakali ni bure.
Ya pili, nadhani ni bora kwa wanafunzi katika vyuo vikuu kukaa katika bweni ya chuo ili wakutane wanafunzi wengine na wawe rafiki. Pia wanaweza kula pale na kusoma pale.
Katika maona yangu, inategemea kabisa kama ni vyema kwa wanafunzi wa shule ya sekondari kukaa katika mabweni au nyumbani pamoja na wazazi wao. Kwa mimi mwenyewe, nafikiri kwamba ilikuwa vizuri sana niliishi pamoja na wazazi wangu niliposoma katika shule ya sekondari, kwa sababu ilitusaidia (wazazi wangu na mimi) kukuza udugu ngumu sana. Udugu wangu na wazazi wangu ni muhimu sana -- ninazungumza na wao karibu na kila siku, na ninatumia ushauri wao kila siku pia. Lakini, kwa wanafunzi wengi, kama Zuri ameshataja, wanahitaji kujifunza kuishi bila wazazi wao. Kwa hivyo, ninafikiri inategemea sana.
Kwa wanafunzi wa chuo, lakini, ninafikiri ni muhimu sana kuishi pamoja katika mabweni, kwa sababu moja ya sababu muhimu sana ya kusoma katika chuo ni nafasi kukutana na wanafunzi wengine ambao wanapenda kusoma, kujifunza, nk. Ni rahisi zaidi kukutana na wanafunzi kama hawa, na kupata nafasi na masomo mbalimbali, kama wanafunzi wanaishi pamoja katika mabweni.
Asante kwa maswali mazuri sana, Mwalimu! Kwanza, nafikiri kawaida kwamba katika shule za upili ni bora kwa watu kukaa nyumbani pamoja na wazazi wao na kaka na dada kwa hapa Marekani. Nafikiri hilo kwa sababu nilipenda sana kukaa na wazazi wangu wakati wa kusoma katika shule ya secondari na nimepata nafazi kuzungumza na wao n.t. Lakini najua pia kwamba pale Afrika Mashariki wanafunzi wengi ambao wanapata nafasi kukaa shuleni wananafasi zaidi kusoma bila kufanya kazi za nyumbani kwa hivyo labda pale ni nzuri zaidi kwa wanafunzi kukaa shuleni kwa shule ya secondari.
Kwa chuo kikuu, nafikiri ni bora kwa wanafunzi kukaa mabweni kwa mwaka la kwanza kwa sababu wanaweza kupata rafiki lakini baada ya mwaka moja itakuwa nzuri zaidi kama wanafunzi wanaweza kuchugua kukaa mabweni au katika nyumba za kukosdisha. Hapa Stanford hakuna wanafunzi wengi wanaweza kulipa bei ya kukodisha nyumba pale Palo Alto kwa hivyo sisi hatuna machuguo. Ningependa zaidi kukaa katika chuo kikuu karibu sana lakini kuwezekana kupika chakula changu peke yangu au na rafiki tu bila kulipa katika "dining hall" au "eating club".
Post a Comment