Sunday, April 13, 2008

Meja na Madarasa Mashurutishwa Katika Vyuo Vikuu

Kutokana na mada ya blogu ya Mwalimu kuhusu mahali ya kuishi ya wanafunzi, ningependa kusikia maoni yao kuhusu masomo katika vyuo vikuu, na jinsi ya kuamua meja. Unafikiri wanafunzi wa chuo wanahitaji kuamua meja moja lini? Hapa Stanford, wanafunzi wanahitaji kuamua meja yao kabla ya kumaliza mwaka wa pili. Unafikiri mwaka wa pili ni mapema mno, au sio? Pia, nje ya meja yao, wanafunzi hapa Stanford wanahitaji kusoma madarasa mashurutishwa mbalimbali, kama IHUM, PWR, nk. Unafikiri madarasa mashurutishwa ni muhimu, au sio? Ningependa kusikia maoni yao.

Tutaonana kesho,
Furaha

4 comments:

Zuri said...

Nafikiri kuamua meja yao kabla ya kumaliza mwaka wa pili ni sawa kabisa. Nafikiri hii kwa sababu kama unasoma kwa vyuo vikuu vya nchi ya Kanada, unapasa kuamua meja kabla ya kuanza masomo ya mwaka wa kwanza! Ni nzuri kusoma kwa miaka miwili kabla ya kuamua meja yao kuona masomo ambayo unapenda. Pia, ni nzuri kusoma madarasa mbalimbali kama IHUM na PWR kwa sababu wanafunzi wengi hawajui kwa kweli kazi watafanya baada ya shule na kama unasoma masomo haya unaweza kuwa mwanafunzi mzima.

Deshka Foster said...

Mimi, nafikiri Furaha ametuuliza maswali mazuri pia!

Kwanza, nafikiri kwamba mara ya kuamiua meja hapa Stanford, kabla ya kumaliza mwaka wa pili ni sawa. Nafikiri inaweza kuwa pia kati ya mwaka la pili lakini kwa sasa si mbaya. Kwa mimi, nilijua kabisa kama nilitaka meja wa Bayologiya wa binadamu wakati wa kuanza mwaka wa pili.

Kwa swali la pili, nafikiri kwamba madarasa mashurutishwa mbalimbali ni kitu kizuri kama IHUM, PWR au SLE. Wanawasiadia wanafunzi kujifunza kuandika n.t. Lakini nafikiri kwamba hapa kuna GREs (General Education Requirements) sana mno. Mimi nimesoma madarasa mengi wa meja mengi lakini pia kuna madarasa ambao sitaki kusoma na ninahitaji kufanya. Ningependa kupata nafasi kuchagua madarasa yangu zaidi.

asanteni na tutuonana baadaye!

-Cheka

Upendo said...

Mimi niliamua meja yangu baada ya kuchague kosi wakati wa kaskazi kuhusu historia na njia ya kuwaambia watu kuhusu kale. Kabla ya kuchukua kosi hii, sikujua kabisa mambo gani za kusoma. Nilikuwa tayari kuamua, lakini sijui kwamba wanafunzi wengi wako tayari wakati wa kumaliza mwaka wa pili. Labda wanahitaji kuchukua kosi nyingine katika idara nyingine kabla kuamua meja yao. Nafikiri si muhimu kujua meja kabla ya mwisho ya mwaka wa pili; wanafunzi wanahitaji kuweza kumaliza madai yao tu.

Kama Cheka alishasema, ninafikiri kwamba madarasa mashurutishwa mbalimbali (kama IHUM, PWR, na SLE) ni muhimu kwa sababu yanawasaidia wanafunzi sana ili waweze kushuhudia masomo mengi kabla ya kuamua meja moja. Nilijifunza mambo mengi kwa sababu nilichukua kosi mashurutishwa. Lakini pia nafikiri serikali (administration?) ya Stanford inahitaji kubadilisha vitu vichache ili madarasa mashurutishwa yanafanya kazi bora zaidi.

Lena said...

Kwa mimi, sina maoni makubwa kuhusu swali hilo, kwa sababu nilienda chuo kikuu tofauti, na sijui mahitaji ya Stanford. Nafikiri chuoni kwangu wanafunzi walilazimisha waamue wakati wa mwaka wa pili pia. Ilikuwa sharti niamue kabla ya kuanza mwaka wa kwanza kwa sababu nilifanya digrii ya kwanza na digrii ya pili wakati wa miaka minne. Nafikiri wanafunzi waamue kabla ya kuanza mwaka wa tatu kwa sababu wanahitaji muda ya kutosha kumaliza mahitaji ya meja yao.

Nje ya meja yao, wanafunzi wasome madarasa yanayoshurutishwa ili wawe wanafunzi mzima, kama Zuri alivyosema. Wanafunzi wanasukumwa kujifunza juu ya masomo tofauti. Pia mahitaji yale yanawasaidia kujifunza ujuzi kama jinsi ya kuandika vizuri.