Sunday, May 18, 2008

Chakula unachopenda zaidi

Ningependa kujua aina ya chakula mnachopenda zaidi. Je, mnapenda chakula cha Marekani au chakula cha nchi nyingine? Mnapenda kula wapi (mkahawa gani?) hapa mji wa Palo Alto? Mnapenda chakula gani cha Afrika Mashariki?

Kwa mimi, nastahiba chakula cha pahali pengine kuliko chakula cha Marekani. Kwa mfano, napendelea vyakula vya Tailandi na Japani sana. Pia napenda vyakula vya Korea na Vietnamu. Kwa bahati njema, naweza kula vyakula hivi hapa pwani magharibi ya Marekani kwa sababu kuna watu wengi waliotoka nchi hizi. Mjini mikahawa inapendwa nami ni Thaiphoon, Fuki Sushi, Zao, Tofu House, Pluto's, The Counter, and Hobee's.

Katika Afrika Mashariki napenda vyakula vengi: hula chapati na mbuzi au chapati na samaki na daima sikumawiki. Pia napenda kula pilau, matoke, na hata ugali. Kwa hakika, matunda ni tamu sana!

Je, mnafikiri nini?

~Maua (Lena)

Monday, May 5, 2008

Upendo's Post

Kitu ambacho unapenda bora kufanya nje ya darasa...

Hamjambo wote! Wikendi hii nilienda katika "campsite" karibu na La Honda pamoja na marafiki wengi kuwa na "counselor retreat" kwa Camp Kesem. "Camp Kesem" ni jina la kambi ambapo ninafanya kazi kila mwaka. Kuna watota mia moja na hamsini na "counselors" (wote ni wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Stanford) sitini ambao wanakuja kambini kwa wiki moja tu kila mwaka. Watoto wote wamekuwa na angalau mzazi mmoja ambaye amekuwa na au ana kansa. Ni wiki muhimu sana kwa watoto na sisi wanafunzi wa chuo pia. Tunakuwa marafiki kwa kweli.

Tangu nilipofika katika Stanford, kambi hii ni kitu ambacho kinapendwa nami zaidi ya shuguli nyingine. Wakati nitaacha kuwa mwanafunzi ya Stanford, nitasikitika sana kwa sababu sitaweza kurudi katika "Camp Kesem."

Na ninyi? Nini ni shuguli kwamba unapenda kufanya bora zaidi nje ya darasa?

Usiku njema na tutaonana kesho!
~Upendo