Monday, November 10, 2008

Filamu ambazo mnapenda bora zaidi?

Tumeshajadili aina mbalimbali ya fasihi. Lakini, aini tofauti ya sanaa ni filamu. Mimi, sijui sana kuhusu sanaa ya filamu na sanaa ya kupiga picha za sinema, lakini napenda sana kuangalia filamu tofauti tofauti. Je, mnapenda kuangalia aina gani za filamu bora zaidi? Mimi, napenda filamu za kitendo bora zaidi. Kwa hivyo, nimefurahia sana kwa sababu wiki hii, filamu mpya ya James Bond itafungua sinemani. Nimefurahia sana kwa sababu napenda sana filamu zote za James Bond, na pia napenda mchezaji mpya wa James Bond - mchezaji mwiingereza anayeitwa Daniel Craig. Napenda filamu za kitendo kwa kawaida, lakini ni muhimu sana kwangu kuwa kuna ishara ya mapenzi pia. Nitaenda kuangalia filamu hii Alhamisi katika saa sita ya usiku! Je, mnapenda filamu za kitendo pia? Au mnapenda aini tofauti kabisa?

Tutaonana kesho,
Furaha