Sunday, April 26, 2009

Riwaya ambazo mngependekeza

Hamjambo wote?  Natumaini mlikuwa na wikendi nzuri.  Kwa mada ya blogu yangu, ningependa kuzungumza kuhusu riwaya ambazo mnazopenda bora zaidi, na pia kuhusu riwaya mmeshamaliza au mnasoma sasa ambazo mngependekeza.  Sasa nasoma riwaya ambayo inaitwa "Midnight's Children."  Mwandishi ni Salman Rushdie, na ana mtindo maalum sana ambaye unaungana sehemu za historia na za uchawi pamoja.  Ndani ya hadithi yake, kuna watu wa wageni sana, na vitu vinaweza kupita ambazo vinatufumba kabisa kama wasomaji.  Hadithi hiyo inafuata maisha ya mmoja ambaye alizaliwa tarehe na dakika kamila Bara Hindi iliposhinda uhuru kutoka Uingereza.  Kwa sababu ya uzaliwa wake maalumu, herufi huyu ana nguvu maalum pia -- na ana kuru ambayo inafanana na kuru ya Bara Hindi zima yenyewe.  Ingawa sijamaliza bado, ningependekeza riwaya hii sana.  

Nasoma pia sasa hivi kitabu kingine (kwa sababu napenda kusoma riwaya mbili au tatu wakati huohuo), inaitwa "We Wish to Inform You That Tomorrow We Will Be Killed With Our Families."  Ni riwaya maarufu sana kuhusu mauaji ya Rwanda.  Mwandishi ni mwandishi habari, na kitabu hiki kinajadili asili za mauaji hayo na historia nyumba ya mauaji, na pia kisa za watu wengi kutoka mauaji.  Sehemu nyingi ni ngumu sana kusoma, na nafikiri kitabu kilitoa picha ya kufahamu sana kusaidia kueleza vizuri zaidi mauaji katika Rwanda.  

Kuna wowote ambaye umeshasoma "Midnight's Children" au "We Wish to Inform You"?  Ulipenda kuisoma?  Ningependa kuzijadili sana!  Pia, ningependa kusilia mnasoma nini sasa hivi na mngependekeza riwaya yoyote?  

Nimefurahia majibu yenu, na tutaonana kesho,
Furaha