Hamjambo wote? Natumaini mlikuwa na wikendi nzuri. Kwa mada ya blogu yangu, ningependa kuzungumza kuhusu riwaya ambazo mnazopenda bora zaidi, na pia kuhusu riwaya mmeshamaliza au mnasoma sasa ambazo mngependekeza. Sasa nasoma riwaya ambayo inaitwa "Midnight's Children." Mwandishi ni Salman Rushdie, na ana mtindo maalum sana ambaye unaungana sehemu za historia na za uchawi pamoja. Ndani ya hadithi yake, kuna watu wa wageni sana, na vitu vinaweza kupita ambazo vinatufumba kabisa kama wasomaji. Hadithi hiyo inafuata maisha ya mmoja ambaye alizaliwa tarehe na dakika kamila Bara Hindi iliposhinda uhuru kutoka Uingereza. Kwa sababu ya uzaliwa wake maalumu, herufi huyu ana nguvu maalum pia -- na ana kuru ambayo inafanana na kuru ya Bara Hindi zima yenyewe. Ingawa sijamaliza bado, ningependekeza riwaya hii sana.
Nasoma pia sasa hivi kitabu kingine (kwa sababu napenda kusoma riwaya mbili au tatu wakati huohuo), inaitwa "We Wish to Inform You That Tomorrow We Will Be Killed With Our Families." Ni riwaya maarufu sana kuhusu mauaji ya Rwanda. Mwandishi ni mwandishi habari, na kitabu hiki kinajadili asili za mauaji hayo na historia nyumba ya mauaji, na pia kisa za watu wengi kutoka mauaji. Sehemu nyingi ni ngumu sana kusoma, na nafikiri kitabu kilitoa picha ya kufahamu sana kusaidia kueleza vizuri zaidi mauaji katika Rwanda.
Kuna wowote ambaye umeshasoma "Midnight's Children" au "We Wish to Inform You"? Ulipenda kuisoma? Ningependa kuzijadili sana! Pia, ningependa kusilia mnasoma nini sasa hivi na mngependekeza riwaya yoyote?
Nimefurahia majibu yenu, na tutaonana kesho,
Furaha
2 comments:
Sijambo Furaha, asante sana. Napenda mada yako - hatujaandika kuhusu riwaya mbalimbali ambazo tunapenda. Sijasoma riwaya za Salman Rushdie, lakini nimesikia vitu vizuri kuhusu uandishi wake. Ningependa kusoma "Watoto wa Jioni" lakini na masomo yangu, hakuna nafasi nzuri kusoma kwa furaha tu. Sasa umemaliza kitabu hiki? Kwa sababu kutoka/kwa (from) elezo lako, ni kitabu kizuri sana! Sasa kuhusu kitabu cha Philip Gourevitch kuhusu Rwanda. Nilisoma kitabu hiki kwanza wakati nilikuwa miaka kumi na tano, katika Rwanda. Nakumbuka kusoma kuhusu Kibuye garini, wakati nilikuwa nikiendesha kwa njia ya Kibuye. Nakubaliana nawe Furaha - hadithi hii ni ngumu sana kusoma. Ijapokuwa najua vitu ambavyo vilitokea katika Rwanda, bado ni ngumu sana kuamini watu wanaweza kuua watu wengine katika damu baridi - marafiki zao, jirani zao, CO-wafanyakazi wao, kadhalika.
Kuhusu vitabu vingine ambavyo nimesoma na nimependa...kuna "Mashiriki ya Eden" na mwandishi ni John Steinback. Ni kitabu kizuri sana. Ni riwaya ambayo inafuata maisha ya kaka wawili kama hadithi ya Cain na Abel katika Biblia. Nani amesoma riwaya hii?
Salama -- Katempa.
Sijasoma Salman Rushdie pia, lakini ningetaka kusoma vitabu vyake kiangazi hiki. Sijasoma "We wish to inform you..." na sifikiri nitakisoma kwa sababu nimesoma vitabu vya kutoshaambavyo vinaeleza mauaji ya Rwanda.
Kuna vitabu vingi ambavyo ninapenda sana. Ninakubaliana na Furaha kuhusu Gabriel Garcia Marquez. Tumejadili Marquez pamoja darasani lakini ninapenda sana vitabu vyake. Pia, ninapenda sana kusome hadithi fupi. Haditihi fupi zangu za kufuraha zaidi zinaandikwa na Hemingway. Napenda sana hadithi fupi zake kama "Three Day Blow", "A Clean Well Lighted Place", na "The Snows of Kilimanjaro".
Sasa ninasoma riwaya fupi za J.D. Salinger kuhusu familia kubwa. Riwaya zake zina"inspired" filmu mengi za Wes Anderson kama "Royal Tennenbaums" na "Darjeeling Express". Kila riwaya ya Salinger kuhusu familia hii, kama "Franny", "Zooey", au "Seymour: An Introduction" inajadili mtoto moja wa familia wao. Ningetaka mnazipenda sana.
Post a Comment