Saturday, January 12, 2008

Uteuzi wa Mgombea wa Urais Marekani

Hamjambo?

Ningependa kusikia maoni yenu kuhusu mada hiyo hapo juu. Kwa wakati huu wanasiasa wengi wa Marekani wanataka kura ili kuchaguliwa kuwa wagombea wa urais wa vyama vyao (Wanademokrasia-Democrats na Wanajamhuri-Republicans). Kwa maoni yako ni nani watateuliwa (will be nominated) na unafikiri ni kwa nini?

7 comments:

Zuri said...

Ninafikiri Barack Obama atakuwa mgombea wa wanademokrasia kwa sababu anaweza kufanya kazi na watu wote wa serikali. Pia, Wamarekani wengi hawapendi kupigana na nchi ya Iraq. Barack hataki kupigana na watu. Kwa mwisho, na kwa kweli, ninafikiri Barack Obama atakuwa mgombea wa wanademokrasia kwa sababu anatabasamu nzuri sana, na anaweza kuzungumza vizuri.

Kwa Wanajamhuri, ninataka Ron Paul kuwa mgombea wake lakini sijui kama watu wengi wanapenda Ron Paul. Ni shida.

Upendo said...

Kama Zuri alishasema, ninafikiri Barack Obama (au "Barack my Socks," kama familia yangu tunasema!) atakuwa mgombea wa wanademokrasia. Watu wengi Wamarekani, hawapendi wagombea wengine, kama Hillary Clinton. Wengi wanafikiri kwamba waweze kumsadiki Obama, laking Clinton ni "kisiasi" mno. Obama ataunga taifa letu.

Vilevile, ninatumaini kwamba John McCain (kutoka Arizona) atakuwa mgombea wa Wanajumhuri kwa sababu yeye ni "wastani." Wamarekani Wanajumhuri, wataona kwamba wanahitagi kuchagua mgombea "wastani" au hawatashinda uchaguzi mwaka huu.

mohochi said...

Kazi nzuri Zuri na Upendo. Wengine mko wapi? Mjadala uendelee basi.

Lena said...

Nafikiri Hiliary Clinton utakuwa mgombea wa Wanademokrasia kwa sababu ameshashinda pale jimbo la New Hampshire. Yeye ana ujuzi na tajiriba kutoka miaka thelatheni alifanya kazi serikalini. Pia watu wengi wanampenda mumewe.

Nadhani John McCain atateuliwa na Wanajamhuri kwa sababu ana ujuzi pia. Alikuwa mwanajeshi mradi watu wengi wanafikiri anajua kuhusu vita. Watu wanahisi kwamba ananyooka.

Hajanuia nani nitampigia kura.

claire said...

Kama Zuri na Upendo, ninafikiri Barack Obama atakuwa mgombea wa wanademokrasia. (Ningekuwa na furaha sana!) Nafikiri atakuwa mgombea badala ya Hillary Clinton kwa sababu vijana wengi sana, kama wanafunzi na wengine ambao (kwa kawaida) hupigi kura, wanapenda sana Barack. (Kama familia ya Upendo, familia yangu inapenda Barack sana. Krimasi, kaka yangu alipokea shati ambayo inasema "Barack n' Roll." Nafikiri kwamba watu wengi wanapenda Barack pia kwa sababu anazungumza kuhusu matumaini mpya kwa Marekani, na angependa kubadilisha sifa ya kimataifi ya Marekani.

Kama Upendo tena, nafikiri kwamba John McCain atakuwa mgombea wa Wanajumhuri, na kwa kweli ningependa McCain kushinda kwa sababu wagombea wengine (katika maoni yangu) ni kicha, hasa Huckabee na Romney. Nitakuwa na ogopa sana kama Huckabee au Romney atakuwa mgombea wa wanajamhuri.

Deshka Foster said...

Kama Zuri na Upendo na pia Clara wameshasema, ninafikiri Barack Obama atakuwa mgombea wa wanademokrasia. Fikiria yangu ni kwanza kwa sababu nafikiri kwamba watu wengi Marikani wanataka wafikiriaji wa nji ya Marikani ita badilisha sana. Obama ni tofauti sana kutoka wagombea kabla yeye...anajua kuzungumza, ana wazo wengi "innovative" (sijui kusema kwa kiswahili) na yeye ni nguvu!
Kwa mimi pia, natumaini kwamba Obama atapata kiti ya mgombea kwa sababu nampenda!

Kusai said...

Ninakubali na watu wengi hapa, ningependa kuwana Barack kama rais wa Marekani. Sijui kwa nini hakushinda katika Nevada lakini alishinda "delegates" zaidi na hii ni muhimu.

Ana bahati njema katika jimbo la South Carolina kwa sababu wanampenda sana pale lakini sijui kama shinda yake pale itakuwa tosha kupata watu wengi nje ya South Carolina ambayo anahitaji kushinda yoyote.