Sunday, May 18, 2008

Chakula unachopenda zaidi

Ningependa kujua aina ya chakula mnachopenda zaidi. Je, mnapenda chakula cha Marekani au chakula cha nchi nyingine? Mnapenda kula wapi (mkahawa gani?) hapa mji wa Palo Alto? Mnapenda chakula gani cha Afrika Mashariki?

Kwa mimi, nastahiba chakula cha pahali pengine kuliko chakula cha Marekani. Kwa mfano, napendelea vyakula vya Tailandi na Japani sana. Pia napenda vyakula vya Korea na Vietnamu. Kwa bahati njema, naweza kula vyakula hivi hapa pwani magharibi ya Marekani kwa sababu kuna watu wengi waliotoka nchi hizi. Mjini mikahawa inapendwa nami ni Thaiphoon, Fuki Sushi, Zao, Tofu House, Pluto's, The Counter, and Hobee's.

Katika Afrika Mashariki napenda vyakula vengi: hula chapati na mbuzi au chapati na samaki na daima sikumawiki. Pia napenda kula pilau, matoke, na hata ugali. Kwa hakika, matunda ni tamu sana!

Je, mnafikiri nini?

~Maua (Lena)

3 comments:

Zuri said...

Mimi na penda zaidi chakula cha nchi ya Kenya. Kama naweza kuanza kila siku pamoja na kikombe kikubwa cha chai, najua siku itakuwa safi sana. Pia, nafikiri kula mandazi au mkate na Blue Band kwa chakula chamshakinywa ni tamu sana. Kwa chakula cha mchana napenda mboga kienyeji cha kabichi. Chakula hii ni tamu zaidi ya vyakula vyote vingine. Kwa chakula cha mchana napenda pia kula kuku na viazi na chapati. Kufika jioni, napenda kula nyama choma na samosa na viazi au wali. Napenda kunywa pombe kama naweza.

Hapa Stanford napenda kwenda kula pale In'n'out na pia hoteli za chakula cha Uchina.

Upendo said...

Mimi mwenyewe, ninapenda sana kula chakula cha Vietnam na Japan. Hapa mjini wa Palo Alto, unaweza kutafuta chakula cha Vietnam na Japan kizuri sana katika mkahawa mingi kama Tamarine, Fuki Sushi, Zao Noodle Bar, na kadhalika. Kuna mkahawa ambapo wapishi wanatayarisha chakula ambacho kinakoroga mitindo mingi pamoja. Kwa kiingereza kinaitwa "Fusion." Mimi napenda sana kula chakula cha "Asian Fusion," na ni maalum sana kwa hivyo watu wanaweza kwenda mikahawani mingi kama wanataka chakula hiki.

Ingawa chakula ambacho ninapenda zaidi ni "Asian fusion," ningekula chakula cho chote. Nimejaribu mitindo mingi na nilipenda karibu na kila kitu. Wakati wa kusafiri ninapenda kujaribu chakula kinatoka pahali tofauti.

Lakini...kwa sababu sina pesa zakutosha kusafiri mara kwa mara au kula nje kila siku, mimi nakula vyakula vya "microwave" kwa kawaida....

-Upendo

Deshka Foster said...

Kama Zuri amesema mimi napenda sana chakula cha Afrika Mashariki. Lakini pia napenda sana kula maboga mengi sana kama "salad" na vitu ambavyo vinasaidia kuwa na afya nzuri.

Wakati nilikuwa mtoto, famalia yangu tumekula chakula kutoka nchi nyingi sana-Mexico, Italia, Chine na kadhalika. Kwa hivyo mimi najua kupika sana kama kutengeneza "sushi".

Kwa sababu nina mzio kwa unga wa ngoma (wheat flour), wakati la kwanza nimeenda afrika mashariki nikaogopa kidogo kwamba haitakuwa vyakula ambavyo nitaweza kula lakini kwa kweli, kuna vitu vingi pale afrika ambavyo naweza kula: wali, nyama choma, ugali, mchicha, kitumbua, n.t.