Thursday, February 26, 2009

Kwa Kutafuta Faraji

Mambo? Natumaini mnaendelea vizuri. Ningependa tuzungumze kidogo kuhusu wazo la faraja. Kwangu, inaonekana kwamba watu wote wako na jinsi yao ya kutafuta faraja wakati wanaipohitaji, na ningependa kujua jinsi yenu ya kuitafuta. Kwangu, wakati nasikia vibaya ama nahitaji faraja, napenda kuenda kupiga picha, ama kuangalia picha zangu za zamani. Pia, nikisikia vibaya kwa mwili, napenda kuenda kukimbia ama kuenda kwa baisikeli wakati nasikiliza musiki. Nikipigisha moyo wangu, najua nitasikia vizuri zaidi baadaye. Kusafisha chumba changu ni jinsi nyingine ya kupata faraja, kwa sababu siwezi kufikiri vizuri ikiwa naona fujo tu. Pia, napenda kuwapigia marafiki zangu simu ama kuenda kuwaona mkahawani ama nyumbani. Mimi ni mtu wa watu, kwa kweli. Napata mwanga kutoka watu wengine wakati ninaposikia nimezungushiwa na giza mimi. Hii ndio maana marafiki zangu ni muhimu sana: wananisaidia wakati ninapokuwa giza, na mimi najaribu kuwasaidia wakati wanapokuwa giza wao.
Najua lakini kwamba watu wengine hawapendi kuhitaji watu wengine kwa kupata faraja, na wangependelea kutafuta faraja kutoka wao wenyewe. Hawapendi kuhitaji mtu mwengine, labda kwa sababu wanaogopa yule ataondoka siku moja, na watakuwa peke yao. Hawapendi kutegemea na watu wengine.
Sijui ikiwa ningeweza kuendelea bila kutegemea na watu wengine, hata ikiwa ningependa kuijaribu. Na ninyi? Mnategemea na watu wengine, ama mnawapenda tu bila kuwategemea? Ikiwa mnategemea nao, mnafanya nini wakati hawapo? Ikiwa hamtegemea nao, mnafanya nini kwa kutafuta faraji (isipokuwa kuitafuta nao)?

3 comments:

Kate said...

Danieli - asante sana kwa fikara yako kuhusu kuhitaji faraji. Nakubali na vitu vingi ulivyoandika na kama wewe, nafikiri marafiki yangu ni muhimu kwa maisha yangu na mimi ni mtu wa watu. Hii si kusema kwamba sipendi kuwa pekee mara kwa mara, kwa mfano baada ya kukaa na marafiki yangu kwa siku yote au wakati nina kazi nyingi, au labda baada ya kusikia habari vibaya. Lakini sipendi kuwa pekee kwa wakati mrefu/ndefu kwa sababu nimetambua kwamba watu au marafiki ambazo wanapenda kusikiliza, kwa kweli wanaweza kunisaidia. Hii ni kwa sababu nimetambua kuhusu mimi kwamba ninahitaji watu kusikiliza tu. Nafikiri watu ambazo wanasema hawahitaji watu wote kufurahia wana matatizo au labda wana wapweke, kwa sababu ijapokuwa ni kawaida kupenda kuwa pekee mara kwa mara, kwa kawaidi binadamu ni watu wa maingiano (social). Uone familia za jamii yote - watu abadi kutafuta kwa watu wengine kuwapenda, kuwaoa, na kuwa na wao tu. Nafikiri unaweza kutegemea watu na ni muhimu kufanya hivi kwa sababu hii ni njia kujenga amana. Ikiwa watu wanahitaji kuondoka, usifikiri wanajaribu kukudhuru. Pengine ni kweli, lakini nafikiri mara nyingi watu wanahitaji kuondoka kwa sababu nyingine na wanakupenda ufurahie. Watu wote wanahitaji kufahamu kwamba binadamu ni watu wa dunia na ni kawaida hatukai katika mahali moja kwa maisha yetu. Ni wazi (evident) kwamba kuna watu tofauti - labda watu wengine wanapenda kuwa na watu wengine mara nyingi na watu wengine wanapenda kuwa pekee mara nyingi - lakini katika mioyo yangu tunatafuta upendo na kupendwa.

claire said...

Njia yangu ya kutafuta faraja inafanana na sana na hizo za Danieli na Katempa. Kama wao, mimi sijali kutegemea rafiki zangu kwa msaada, na napenda sana kuzungumza sana na rafiki zangu bora zaidi. Ni muhimu sana kwangu kuweza kuzungumza na familia yangu - hasa wazazi wangu na dada yangu - kuhusu maisha yangu na matatizo yoyote. Mimi ni wazi sana na wazazi wangu, na tunaweza kuzungumza kuhusu vitu ambavyo watu wengi hawapendi kujadili na wazazi wao (kama wapenzi, na kadhalika). Kwangu, siogopi kutegemea watu wengine, kwa sababu najua (kama Katempa na Danieli) kwamba naweza kusikia vizuri zaidi peke yangu, bila msaada wa watu wowote. Lakini, mara kwa mara napendelea kuzungumza kuhusu shida zangu. Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kwamba inanisaidia kuelewa moyo yangu na njia ya kutengeneza shida.

Kutafuta faraja, kama Danieli napendi kwenda kufanya mazoezi mazingirani. Inanisaidia kwenda mahali pazuri, kama katika kilima ambacho kiko karibu na Dish. Napenda sana kusikiliza muziki pia ninapofanya mazoezi au ninapokwenda kwa baiskeli. Napenda sana pia kusoma riwaya mbalimbali kutafuta faraja ninapokuwa na wasiwasi. Hata nikichoka sana, nasikia vizuri zaidi ninaposoma kabla ya kwenda kulala usiko. Lakini, kama nimeshasema, msaada mkubwa sana kwangu unatokea rafiki zangu na familia yangu.

Kusai said...

Katika maisha yangu, napata faraja kutoka vitu ambavyo vinanishughulika, kama Danieli na picha zake. Napenda sana kusoma na kuandika hadithi fupi. Kitabu changu za kufurahia zaidi ni "Miaka Mia ya Upweke". Ninapenda kutafuta faraja katika kitabu hiki au kutoka waandishi kama Hemingway (napenda hadithi fupi zake), J.D. Salinger, au Nietzsche (yeye ni zuri sana kama nahitaji kupata faraja katika maisha yangu).
Pia ninakubalia na Danieli kuhusu chumba changu. Siwezi kufikiri wakati chumba changu ni vuruguvurugu. Kweli, napenda sana kusafisha. Ninafikiri ni jinsi nzuri ya tulivu kupata salaam.
Kama watu wote pia, napenda kutulia na marafiki yangu. Tunapenda kucheza ngozi kutafuta faraja.
Nafikiri wazo zetu kuhusu faraja zinafananana sana.