Sunday, May 10, 2009

Hadithi Nzuri Kutoka Wikendi Ya Mwaka Huu

Hamjambo wote! Habari za wikendi yenu? Nilienda mji wa San Francisco kukutana na rafiki yangu mpya -- Sabbo. Yeye ni DJ kutoka mji wa Tel Aviv. Kwa sababu nilijifunza kufanya kazi ya DJ wakati nilisoma mji wa Oxford pale Uingereza, nilifurahia sana kukutana Sabbo Alhamisi iliyopita katika karama huko San Francisco. Anakaa hapa (San Francisco) kwa miezi miwili kwa Lebo ya Record yake. Anafanya kazi ya DJ katika karamu mbalimbali mjini mpaka kati ya Juni. Tulizungumza kidogo na nilimwliza ikiwa niliweza kutumia vifaa vyake kuboresha uzoefu (skills) wa DJ wangu. Alikubali, na Jumamosi, Sabbo aliniruhusu kucheza na vifaa vyake and kuchanganya nyimbo pamajo. Kila wakati nina nafasi kufanya kazi hii, kweli nafurahia sana. Si rahisi - unahitaji kufikiri nyingi and kuweza kusikiliza nyimbo mbili kwa wakati mmoja (at the same time). Lakini unapopita curve ya ujifunzo, ni safi sana kwa sababu unaweza kuwa na karamu nzuri na kuwastarehesha watu wengi! Ikiwa sikuhitaji kutengeneza pesa kuishi, nafikiri ningenunua vifaa na ningejifunza kuwa DJ safi sana. Hii ingekuwa mradi wa mmoja kwa sababu pia ningependa kujifunza kutoa muziki, kama DJ za Diplo, Girl Talk, Sabbo, kadhalika. Sabbo nami tulikuwa marafiki haraka na nitarudi San Francisco wiki hii kuchill naye zaidi. Pia - nilijifunza asubuhi kutoka rafiki yangu ambaye anatoka Israel kwamba Sabbo ni mtu maalum sana huko. Ana kundi linaitwa "Soulico" na wanamaliza CD ya kwanza wao siku hizi. Je, mna hadithi safi sana kuhusu wikendi iliyopita? Labda hakuna hadithi kutoka wikendi hii, lakini pengine kuna hadithi kutoka wikenda ya mwaka huu ambazo hamkuambia?

1 comment:

Kusai said...

Ijumaa iliopita marafiki zangu nami tulifany sherehe kubwa. Sisi ni viongozi vya shirika la wanafunzi wa masomo ya mahusiano ya kimataifa na tulikuwa na pesa nyingi ambazo tulihitaji kutumia muhula huu, kwa hivyo tuliamua kuzitumia kupata vileo, musiki, na chakula nzuri zaidi za sherehe zote za chuo kikuu. Siwezi kusema dola ngapi tulilipa, lakini sherehe yetu ilikuwa nzuri sana.

Tulianza na chakula cha jioni kutoka Whole Foods. Nilisisimuwa kupata vileo vinaitwa "Chartreuse" na "Eau de Vie". Chupa yetu ya Eau de vie inafanyiwa na mapeasi tu. Pia kuna peasi nzima katika kila chupa ambao inapandwa, juu ya mti, katika chupa kabla ya kuunga kileo cha "Eau de vie".

Tulijaribu kufanya ujadili kuhusu bei za masomo katika chuo kikuu cha Stanford lakini ninafikiri watu wengi, pamoja na mimi, walikunywa sana kwa hivyo hawataki kusikiliza. Labda Katempa anaweza kueleza bora zaidi kuhusu ujadili.

Katempa alikuja na marafiki zake na waliimba sana. DJ yetu, anaitwa "DJ Purple", anafanya musiki ya karaoke kwa hivyo kila mtu aliokuja aliimba na alicheza. Hata baada ya kunywa vileo vingi, Katempa aliimba nzuri sana. Mimi niliimba nyimbo nyingi kama "Marafiki katika nafasi za chini" na Garth Brooks na "Juicy" na Notorious BIG.

Ilikuwa sherehe nzuri ninafikiri na kila mtu anaokuja alifuraha sana.