Monday, November 12, 2007

Wikendi iliopita yangu

Nilienda mji wa Philadelphia na timu yangu ya Model UN kuzumgumza mahusiano ya kimataifa na nimefurahi kabisa. Wakati tuliondoka nilikuwana uoga (au wasiwasi) sana kwa sababu mimi ni kiongozi cha timu kwa hivyo nimehitaji kuyakini (to be sure) tulienda na tulikaa hotelini na tulikula na tulirudi bila shida. Nilikuwa na wasiwasi lakini sasa imemaliza na ninaweza kurudi chuoini na kufanya kazi yangu ya nyumbani. Ilikuwa nzuri kabisa na ninafikiri watu wote katika timu ya Model UN wamefurahi.

5 comments:

mohochi said...

Habari zenu wote?

Nafurahi kuona kwamba wengi wenu manaandika katika blogu. Sasa hata mimi ninajua mlichofanya katika wikendi. Je, Zuri wewe hukufanya chochote utwambie? Mimi nilikuwa na shughuli nyingi sana kwa sababu nilikuwa ninahama kutoka kwa nyumba moja hadi kwa nyingine. Sikuwa na huduma za mtandao mpaka jana jioni na hilo limetatiza mno kazi zangu.

Nafurahi pia kuwa mmeanza kujadili kuhusu mada ya wasilisho la kitamaduni la muhula huu. Mada ambayo mmependekeza ni nzuri kwa hivyo tuendelee kupanga tu.

Baadaye.

Furaha said...

Kusai, nimefurahi sana kusikia kwamba wikiendi yako na Model UN iliendelea vizuri sana.

Mimi, nimefurahia sana, kwa sababu nitarudi mji wa Seattle kutembelea familia yangu kule kwa likizo ya Thanksgiving. Nitaondoka jumamosi, na sitarudi mpaka jumatatu ya wiki kesho kutwa, kwa sababu sikuweza kupata usafiri kwa ndege katika jumapili baada ya Thanksgiving. Nimefurahia sana kuwaona mama, baba, na dada yangu. Kaka yangu, lakini, sitamwona Seattle kwa sababu atakaa na familia ya mpenzi wake kwa likizo yote. Sijafurahi, kwa sababu sikumwona tangu kabla nilienda Tanzania kiangazi kilichopita, mwezi wa sita mwaka huu, na kwa sasa sitamwona mpaka likizo ya Krismasi. Lakini, nitakuwa na furaha sana kukaa na familia yangu kwa wiki zima. Je, mtafanya nini kwa likizo? Mtarudi nyumbani au mtakaa hapa chuoni?

Tutaonana baada ya likizo!
Furaha

mohochi said...

Nawatakia nyote safari njema wakati wa likizo ya kutoa shukrani. Mimi sitaenda popote. Nitakuwa hapa hapa na nitatumia wakati huo kufanya kazi zangu za utafiti. Itakuwa vizuri ikiwa mtaandika katika blogu kuwafahamisha wengine mambo yanavyoendelea katika likizo. Mlisema naweza kumualika Furaha kujiunga na blogu ili aweze kuanzisha mada kwa kufanya nini?

Kwaherini.

Furaha said...

Asante mwalimu, na tunakutakia likizo njema pia. Nafikiri kwamba, kwa sababu wewe ni mwandishi wa blogu hii, utakapoingia blogu, unaweza kwenda ukurasa ambayo ina mamlaka ya blogu, na halafu unaweza kunikaribisha tena. Samahani sana kwa kunisababisha kazi zaidi!

Likizo njema wote!
Furaha

Furaha said...

Samahani, nilimaanisha kusema "samahani sana kukusababisha kazi zaidi" badala ya kunisababisha. Nimechoka, nafikiri...

~Furaha